Sunday, April 30, 2017

WAJINGA NDIO WALIWAO; Hekaya za Abunuwasi

TUJIKUMBUSHIE HEKAYA ZA ABUNUWASI Paliondokea mtu katika kisiwa cha Unguja, enzi za Seyid Majid Bin Said, naye akikaa mjini. Na mtu huyu alikuwa hana kazi maalum, kazi yake ilikuwa ni kuwafuata Waarabu wakubwa wakubwa, na kupata manufaa yake kwao. Na kazi zamani hizo ilikuwa watu kufunga bidhaa na kwenda bara kufanya biashara, na kulima vyakula na kuuza. Na yeye alikuwa mtu mmoja asiyetaka kazi ya namna hii. Hata hatima akaonelea mji haumweki. Akatafuta kanzu yake njema akavaa, na kilemba chake cheupe, na msahafu wake kwapani, akashika njia kwenda pande za mashamba kutarazaki. Na kazi aliyoichagua ni kazi ya ualimu kusalisha watu. Lakini yeye hajui kusoma hata herufi moja. Alichagua kwenda shamba kwa Wahadimu kwa kuwa huko ndiko walikokuwa wajinga wasiojua kusoma, na hata dini ya Kiislamu ilikuwa haijaingia kwao bado. Basi Mwalimu akawasili Unguja Ukuu. Wahaimu walipomwona mgeni wakamkaribisha sana. Hata waliposikia kuwa yeye ni mwalimu wakazidi kumkaribisha na kumheshimu. Na yeye mwenyewe ikawa mchana kutwa kufunua msahafu, kutazama tu, watu wanadhani anasoma! Akapewa nyumba bure na chakula kwao. Hatima akawaambia, Jengeni msikiti nikusalisheni. Wahadimu wakajenga msikiti. Hata wakati wa kusali ulipojiri mwadhini hapana, maana wale wenyeji hawajui. Basi ikawa kazi ya mwenyewe Mwalimu kuadhini. Lakini naye vilevile hajui kitu. Akasimama akaadhini hivi:- Allah Akbar! Allah Akbar! Wajinga ndio waliwao, Wajinga ndio Waliwao. Allah Akbar ! Watu wakajaa msikitini. Huyu mwalimu kama nilivyosema hajui kusoma, si kukuambia kusalisha! Lakini watu wamekwisha kuwamo msikitini, ikawa hana hila ila kusalisha. Akaenda panapo Kibla, akasalisha hivi:- M, m, m,m ,m,m Wajinga ndio waliwao, Amin. Ikawa kila akisema M,m,m ,m,m ,m ,m Wajinga ndio waliwao, Wajinga ndio Waliwao, Wahadimu huitikia Amin! Ikawa kila akiinama na kuinuka maneno ni hayo hayo. Na Wahadimu wakidhani asema Kiarabu, wakawa wamekazana tu, Amin! Zilipokwisha sala wakatoka nje. Wahadimu wakamsifu sana mwalimu wao jinsi anavyosalisha vizuri. Ikawa hivi hali ya mambo kwa siku nyingi kupita. Wakamfanyia mshahara mwema. Siku moja akatoka Malimu wa kweli mjini anayejua kusoma na kusalisha ili kwenda kutembea shamba. Akafika Unguja Ukuu. Akapata habari kama mjini pana Mwalimu mmoja arifu sana, ndiye anayesalisha msikitini. Na huyu mwalimu mgeni asiende kumtazama, akangoja mpaka wakati w sala. Wakati wa sala ulipojiri akamsikia mwadhini anaadhini. Lakini maneno yake yakamstusha sana. Allah akbar! Allah akbar! Wajinga ndio waliwao. Allah akbar! Yule mgeni asiseme neno, akaenda msikitini, akakuta watu wamejaa. Na mbele yao panapo kibla yuko mtu anayemjua tangu mjini, naye kumjua kwake hajui kitu. Basi akamsogelea kule kule mbele ili amsikilize vema. Na mwalimu alipomwona huyu mgeni akastuka sana maana naye amjua tangu mjini. Akawaza kuwa leo uongo wangu utabainika. Lakini mara akili zikamjia hivi:- M,m,m,m,m Mwalimu usinibaini, nikipata sita, tatu zangu, tatu zako, Wajinga ndio waliwao Amin! Na maneno haya wakisikiana wao wawili tu, maana walikaaa karibu karibu. Akashika kusalisha kwa maneno yale yale. M, m,m,m,m,m Mwalimu usinibaini, Wajinga ndio waliwao, nikipata nane, nne zangu na nne zako, Amin. Akasalisha hivi mpaka mwisho, wakatoka. Walipotoka nje wale walimu wakaamkiana kwa vicheko sana. Watu walipowaona wanacheka,wakidhani wanacheka yao ya huku nje, maana wanajuana. Kumbe wanacheka yaleyale ya Msikitini: Mwalimu usinibaini, wajinga ndio waliwao, nikipata nane, nne zangu, nne zako. Wakakaa katika hali hii wakiwala wajinga, mpaka walipochoka, wakaja zao mjini na wingi wa mapesa. Hadithi hii inatufundisha nini? na hali ya Tanzania tukiangalia hali halisi ya uwekezaji feki pamoja na

KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME

HEKAYA ZA ABUNUWASI ni kitabu cha hadithi za kusisimua, zinazofurahisha sana kutokana na umahili wa watunzi wa vitabu vya kale. Kutokana na utamu wa hadithi za ABUNUWASI, Blog ya MOGHA itawaletea hadithi hizo ili kuwachangamsha akili............... KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni, walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama ya mbili. Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni. Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu. Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika haraka eneo la tukio. Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa ulikuwa mkono wa ajabu na uliwekwa na watu wenye imani za kishirikiana, alitoa siku tatu mkono huo uwe umeondolewe, vinginevyo ataleta wataalam kutoka sehemu mbali mbali duniani kwa ajili ya kubaini wahusika. Siku tatu zilizowekwa na Mfalme zikaisha, wataalam wa mambo ya asili kutoka sehemu mbali mbali duniani wakaanza kuwasili mtoni hapo kwa lengo la kuundoa mkono huo wakashindwa. Mfalme akatoa ofa nono, waganga wenye sifa na jeuri ya mambo ya jadi wakamiminika eneo la mto, wakafanya mitambiko na mambo yao kwa ufanisi zaidi, wengine wakalala mtoni kuonyesha umahili wao lakini wakashindwa na kuuondoa mkono huo wa ajabu... Mfalme na wasaidizi wake wakakuna vichwa, wananchi hawana jinsi ya kupata maji. Maji mtoni hayachoteki, wananchi wanaogopa kutumia maji hayo. Ndipo Abunuwasi akajitokeza mbele ya Mfalme. Akamwambia Mfamle, "Mimi naweza kujaribu. Mfalme akamfukuza Abunuwasi kwa hasira, akamwambia. "Mpumbavu sana wewe, hapa wameshindwa waganga na waganguzi, wewe Abunuwasi utaweza wapi, usitupotezee muda wetu". Abunuwasi akaondoka, waganga wakazidi kumiminika mtoni wakitoka sehemu mbali mbali za dunia kutokana na sifa zao. Kila walichofanya kuuondoa mkono huo wakachemka na kuondoka eneo hilo kimya kimya. Abunuwasi akamrudi Mfalme, akamwambia, "Wacha nijaribu mimi". Mfalme akamjia juu akamwambia. "Nimesema huwezi Abunuwasi, wameshindwa waganga wa dunia, utaweza wapi wewe?, Abunuwasi akasisitiza. "Wacha nijaribu mimi kama walivyojaribu wengine na kushindwa. Mfalme kwa hasira akamwambia Abunuwasi, "Haya jaribu, maana unataka kutupotezea muda tu hapa, lakini ole wako ukishindwa, nitawaamru askari wakutie ndani". Abunuwasi akaanza kuuzunguka mto huku umati wa wananchi ukimwangalia kwa makini, alipita huku na huku akikimbia kama mtu aliyepatwa na wazimu, Mfalme akaanza kuchukia, hatmaye Abunuwasi akakaa sambamba na mkono ule, Abunuwasi akachuchumaa chini na kuinua mkono wake juu mfano wa mkono ule. Mfalme na wananchi walikuwa kimya wakifuatilia kwa makini tukio hilo, Abunuwasi aliuchezesha mkono wake kushoto na kulia, mkono ule ndani ya maji nao ukafanya vile, kama alivyofanya Abunuwasi. Wananchi wakashangazwa mno na kitendo kile. Abunuwasi akauvuta mkono wake nyuma, mkono huo pia ukafanya hivyo, Abunuwasi akakunja kidole chake kimoja, mkono ndani ya maji nao ukafanya vile. Hatmaye Abunuwasi akaushusha mkono wake chini kama anaudhamisha, mkono ule nao ukadhama na haukuonekana tena. Mayowe, vigelegele na shangwa vikasikika, Mfalme akasimama akamfuata Abunuwasi, akamuomba radhi, akamtukuza na kuonyesha kufurahishwa. "Ahsante sana Abunuwasi, umetuondolea aibu, nisamehe kwa kukudharau, sikutegemea kabisa". Wananchi wakaja juu wanamtaka Abunuwasi apewe Ufalme. Maana ameweza kufanya jambo lililowashinda waganga na waganguzi. Mfalme akahamaki. Abunuwasi akaula...

Monday, October 10, 2016

Kazi kwenu akina mama. Hebu cheki video.


NECTA yatoa ratiba ya ukaguzi wa vyeti mkoa kwa mkoa.

NECTA yatoa ratiba ya ukaguzi wa vyeti mkoa kwa mkoa. By Daud P. Mogha October 10, 2016 - 10:52


Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.



Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika mkoa, halmashauri na manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

RATIBA YA UHAKIKI

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.

JOTO LA UHAKIKI

Kabla Baraza la Mitihani halijatangaza ratiba hiyo, tayari watumishi wa umma ambao wanatumia majina matatu lakini vyeti vyao vya elimu vinasomeka majina mawili walikuwa wamepewa maelekezo ya kwenda kutafuta hati ya kiapo kwa ajili ya kuapa mahakamani ili kuthibitisha majina yao.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili mmoja wa watumishi hao alisema: “Wakati tunaanza kazi sisi ambao vyeti vyetu tulikuwa tunatumia majina mawili shuleni, tuliambiwa tutumie matatu ambayo pia yanatumika hata kwenye ‘salary slip’, sasa tumeambiwa tunatakiwa kwenda mahakamani kuthibitisha.”

Alisema zoezi hilo tayari limeleta changamoto kubwa mbali na kuzua hofu kwa baadhi ya watu ambao taarifa zao za kitaaluma hazipo sawa sawa.

“Mimi binafsi sina hofu zoezi linakwisha kesho lakini kinachoniuma ni kwamba hiyo hati ya kiapo (affidavit) tukienda Mahakama ya Mwanzo tunaambiwa ni lazima tulipie shilingi 10,000 na kibaya zaidi hatupewi risiti lakini kwa watumishi wengine ambao wanafahamiana wanapata huduma bure,” alisema mtumishi huyo.

Tangu Serikali itangaze kuwafuatilia watumishi wake wote wenye vyeti feki hali ya wasiwasi na sintofahamu imetawala miongoni mwa vigogo, maofisa na watumishi wengine ambao vyeti vyao vya kitaaluma haviko sawa sawa au haviendani na kazi au nyadhifa wanazoshikilia.